MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AIPONGEZA KAMPUNI YA TAMOBA.
Mkuu wa mkoa wa dar es salaam aipongeza kampuni ya TAMOBA kwa kushiriki vema katika mchango wake wa kufanikisha zoezi la upimaji wa afya na matibabu kwa wananchi wote walioko mkoa wa dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa dar es salaam MHE.Paul Makonda Akitoa pongezi ya cheti kwa Mkurugenzi wa Tamoba |
Nae Balozi mstaafu brigedia general Francis Benard Mndolwa Makamu Mwenyekiti Wa bodi ya Ushauri ya TAMOBA ,Ametoa pongezi kwa jitihada za Mkuu wa mkoa wa dar es salaam na kuwataka wakuu wa mikoa mingineyo kuiga mfano wa MHE.Paul makonda kwa kuwajali wananchi wa mkoa wake kwa kuwaletea huduma ya afya check na matibabu iliyotolewa bure.
Pamoja na pongezi hizo Balozi mstafuu wa jeshi la wananchi wa Tanzania,Brigedia general Francis Benard Mndolwa Akiwa kama makamu mwenyekiti wa kampuni ya TAMOBA amesema kuwa Kampuni ya TAMOBA itaendelea kuunga mkono juhudi zote za Mkuu wa mkoa wa dar es salaam katika jitihada za kusaidia watanzania wote
Aidha Mkuu wa mkoa MHE.Paul christian makonda,Amewapongeza madaktari na wote walioshiriki katika kuchangia katika zoezi la upimaji wa magonjwa kwa wananchi wasiojiweza bila kuchangia gharama yoyote.
Vile vile katika shughuli hiyo,MHE.Paul Makonda amewashukuru sana wananchi wenye moyo wakujitolea katika kutimiza zoezi hili na kugawa vyeti kwa wale wote waliotoa mchango wa namna yoyote katika siku ya kutoa matibabu kwa wananchi wasiojiweza iliofanyika jijini dar es salaam katika viwanja vya mnazi mmoja.
Post a Comment