Meja amewaonya askari



Meja Jenerali Michael Isamuhyo ametoa wito huo, wakati alipokuwa akivizindua rasmi vikosi vya 846 KJ Luwa na kile cha 847 KJ Milundikwa, kwenye wilaya za Nkasi na Sumbawanga mkoani Rukwa, na kuonya kuwa askari yeyote atakayejihusisha na vitendo vya unyanyasaji atachukuliwa hatua kali za kinidhamu, kwani lengo la kuwepo kwa vikosi hivyo ni kuleta maendeleo ya haraka kwa ushirikiano wa jeshi hilo na wananchi kwa ujumla.
Kwa upande wao wakuu wa wilaya za Nkasi B.w Said Mtanda na yule wa Sumbawanga Bw. Khalfany Haule, wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa matukio hayo ya uzinduzi wa vikosi, licha ya kusema kuwa kuwepo kwa vikosi hivyo kuna manufaa ya kiuchumi kwa vijiji vilivyo jirani, na pia kuongezeka kwa walimu na wataalamu wengine kwa ajili ya huduma mbalimbali vijijini, lakini pia wamesema kuna umuhimu mkubwa wa kubainisha mipaka ili kusiwepo na migogoro.Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo amewaonya askari vikosi vya JKT nchini na kuwataka kuweka mazingira mazuri na rafiki kwa wananchi wa vijiji vinavyopakana na kambi zao badala ya kuwanyanyasa na kusababisha migogoro