Kitila Mkumbo ajitoa ACT-Wazalendo

Katibu mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo, amejiuzulu uanachama wa ACT-Wazalendo baada ya kudai anapata ugumu kutumikia vitu viwili kwa pamoja.
Katika Barua ambayo imetolewa leo na kusambaa mitandaoni ambayo Kitila Mkumbo amekiri ni ya kwake, amesema kwamba ameona kuna mgongano wa kimaslahi anaoupata kwa kutumikia Ukatibu Mkuu wa wizara, huku akiwa amevaa uanachama cha ACT- Wazalendo.
"Katika maelezo niliyoyaandika hapo juu na ili kuepuka mgongano wa wazi wa maslahi, nimeamua kung'atuka uanachama wangu wa ACT- Wazalendo, kuanzia terehe iliyoonyeshwa chini ya barua hii", ilisomeka sehemu ya barua hiyo.
Kitila Mkumbo amesema uamuzi zaidi anauachia uongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, na huku akiwashukuru kwa ushirikiano kwa muda wote ambao walikuwa kwenye chama.