Dodoma yapiga marufuku
Halmashauri ya wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma palipo na ikulu ya Rais, imesema itawachukulia hatua za kisheria abiria wote wanaopita katika barabara kuu ya Dodoma Morogoro pale watakapokutwa wakirusha takataka wakiwa ndani ya vyombo vya kusafiria.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Godfrey Mnyamale, amesema hayo wakati akizindua zoezi la uwekaji wa mapipa ya takataka katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo vikiwemo vijiji vya buigiri, chinangali na mwegamile kata ya buigiri sambamba na kuweka mabango ya tahadhari kwa wapiti njia lengo likiwa ni kuimarisha mazingira katika hali ya usafi.
"Tunajua kama binadamu kuna kwenda kuchimba dawa lakini tunataka kuwajulisha kuwa lazima wafuate utaratibu wa hapa ikiwa ni pamoja na kuyaacha mazingira yetu kuwa safi ili watu wetu wasipate magonjwa ya mlipuko. Kuna vyoo vya kulipia vipo pamoja mapipa ya kutupa takataka hivyo walinde mazingira yetu" Bw. Mnyamale.
Naye diwani wa kata ya Buigiri, Keneth Yindi, amewahimiza wapita njia kuchukua tahadhari pale wanapopita maeneo hayo ili kuepuka usumbufu pindi watakapokamatwa kutokana na kutupa taka ovyo na kusema faini ni shilingi 50000.
Post a Comment