Dkt. Mwakyembe atoa mbinu ya kutibu Saratani

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewaomba watanzania kutambua kwamba saratani ya matiti inaweza kutibika hivyo ni wajibu wao wa kuhakikisha kwamba wanajiwekea utamaduni wa kuchunguza afya
ili waweze kupata matibabu mapema kama watagundulika kuwa nayo.
Dkt. Mwakyembe amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipoongoza matembezi 
ya
 hisani ya kuchangisha fedha kiasi cha shilingi milioni mia moja zitakazosaidia matibabu
kwa wagonjwa wenye saratani ya matiti hususani wakina mama ambapo matembezi hayo yameandaliwa na Tanzania Breast Cancer Foundation.
Aidha Dkt. Mwakyembe amebainisha kwamba serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa 
kutibu 
saratani ya matiti kutokana na wengi waliokuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo kushindwa 
kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara.