AFISA ELIMU MKOA WA DAR ES SALAAM AHAIDI KUZITATUA KERO ZINAZOWAKABILI WAMILIKI WA SHULE BINAFSI
Afisa elimu wa mkoa wa Dar es salaam akizungumza na washiriki wa mkutano uliowakutanisha wamiliki wa shule binafsi mkoa wa Dar es Salaam,(picha zote na John Luhende)
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa shule binafsi (TAMONGSCO), Charles Totela Akizungumza na wamiliki wa shule binafsi,hawapo pichani
Miongoni mwa wamiliki wa shule binafsi pamoja na wawakilishi waliofika kwenye mkutano huo
Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Hamis Yusufu Lissu , ameahidi kutatua kero zote zinazowakabili baadhi ya wamiliki wa Shule Binafsi mkoa huo ikiwemo ya tozo kubwa za biashara zinazotozwa shule hizo .
Pia amewaomba wamiliki wa shule hizo kipindi cha likizo wajitolee kuwafundisha masomo ya sayansi wanafunzi wanaotoka shule za serikali kwa kuwa wana walimu wengi wa masomo hayo.
Ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua Mkutano Maalumu uliowakutanisha wadau mbalimbali na wamiliki wa shule zilizopo mkoani humo.
Amesema wamiliki wa shule hizo pamoja na shule zao wanapaswa watambaue huduma wanazopewa ni stahiki hivyo ni sawa wanazopatiwa shule za Serikali.
“Natamani kuziona shule zote binafsi zikiwa zinazoongoza kutokuwa na changamaoto zozote kwani tunatambua mchango wa uwekezaji hapa nchini,” amesema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi nchini (TAMONGSCO), Charles Totela ameishukuru Serikali ya mkoa huo kwani imekuwa ikiwapa ushirikiano wa kutosha.
Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali ya mkoa huo kuwaundia dawati la pamoja litakalowakutanisha viongozi wote wa shule binafsi, za serikali na watendaji wao ili waweze kukaa pamoja na kujadiliana baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa hazifanyiwi kazi.
Naye Mkurugenzi wa Shule za Al-Muntazir, Mahmood Ladak amewashukuru wamiliki wa shule hizo kwa kuitisha mkutano huo ambao anataraji utakuwa na manufaa makubwa kwao na taasisi wanazosimamia katika kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Post a Comment