Yanga kuondoka kesho
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC kinatarajiwa kuondoka kesho Ijumaa kuelekea mjini Songea tayari kwa mtanange wa ligi hiyo utakaopigwa Jumamosi hii katika dimba la Majimaji.
Kikosi hicho ambacho tangu kimeifunga Njombe Mji FC Jumapili iliyopita, kiliamua kubaki Njombe, kimekuwa kikiendelea kujifua kwa mazoezi makali kuhakikisha kinachukua pointi tatu nyingine baada ya zile zilizopata kwa Njombe Mji FC.
Daktari wa timu hiyo, Edward Bavu amethibitisha kuwa wachezaji wote wapo katika hali nzuri.
Post a Comment