TEGETA, DAR: Meja Jenerali Mstaafu wa JWTZ, Vicent Mritaba apigwa risasi 5 na majambazi
Majira ya saa kumi kuelekea kumi na moja nilikuwa na kazi fulani mitaa ya Ununio, kuna hotel moja nilikuwa naingia pale. Nikiwa karibu na hii njia inayoingia kwa watengeneza chumvi nimesikia milio kadhaa ya risasi ikirindima na baadaye nikapitwa na pikipiki mbili aina ya Boxer zikiwa speed kali vibaya mno zikiwa na wanaume wawili wawili ingawa sikuweza ona kama wamebeba silaha.
Hivi narudi nipo mitaa ya Giraffe Hotel ndio napata story kuwa kuna majambazi wamempiga risasi afisa wa Jeshi na kawahishwa Hospital.
My Take:
Binafsi nadhani Mahita alipaswa mshauri Sirro namna ya kukabiliana na uhalifu huu wa silaha ambao unazidi tamalaki hapa nchini. Bado nina imani na TISS naamini haya yana mwisho.
UPDATE:
Kwa mujibu wa pansophy,
Meja Jenerali mstaafu wa JWTZ, Vincent Mritaba amepigwa risasi 5 na watu wasiojulikana akiwa anaingia nyumbani kwake, Tegeta Dar es Salaam ambapo watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wamemshambulia kwa risasi Meja Jenerali huyo
Tukio hilo limetokea jioni ya September 11, 2017 wakati Meja Jenerali Mritaba akiwa anaingia getini nyumbani kwake Tegeta ambapo alivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa risasi tumboni, begani na mguuni.
Hadi usiku wa jana Madaktari walikua wanaendelea na upasuaji kutoa risasi tatu tumboni na kushughulikia majeraha mengine katika hospital ya Lugalo.
Rais Magufuli amefika hospitali ya Lugalo kumjulia hali
Post a Comment