Taarifa Kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa mwili wa marehemu Praiveti Mussa Jumanne Muryery ambaye ameuawa nchini DRC akiwa katika jukumu la Ulinzi wa Amani, utaagwa kwa heshima tarehe 25 Septemba 2017 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa        Dkt.  Florens M. Turuka ataongoza katika kuuaga mwili wa Marehemu.

Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi Amin.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano