Ndugai: Sio kila kitu huandikwa, adai atatumia mamlaka yake kadri anavyodhalilishwa
Spika wa Bunge, Job Ndugai akihojiwa na Azam Tv, ameelezea mkutano wa nane kwa ujumla. Ndugai amesema hana ugomvi na Zitto, Lema wala Kubenea na wala hatarajii kuwa nao hata siku moja na ameomba waulizwe wao tatizo ni nini.
Kuhusu uwezo wa kumzuia Zitto kumzuia kutozungumza chochote katika kipindi chake chote cha Bunge, Ndugai amesema sio kila kitu huandikwa katika mahusiano ya kikazi lakini kiongozi wa kazi ana mamlaka makubwa kuliko yaliyoandikwa.
Ndugai amesisitiza japo watu wanabisha bisha, anao uwezo kama spika. Amesema zipo kanuni kwa spika kadri anavyoona inafaa, kwa busara yake namna gani aongoze Bunge.
Amedai haiwezekani mtu akatukana Bunge, akamtukana Spika alafu huyo huyo ampe nafasi ya kuzungumza ilhali yeye sio Malaika, ana damu na nyama kama binadamu wengine.
Kadri anavyonyanyaswa na kudhalilishwa mbele za watu naye atatumia madaraka yake aliyopewa na nchi, na Mungu kuona nini afanye katika mamlaka aliyonayo.
Post a Comment