Snura atafuta wa kumpa mimba

Msanii wa bongo fleva, Snura Mushi maarufu kama Malkia wa uswazi ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa 'zungusha' amefunguka na kudai anatamani kupata ujauzito ila hamtamani atakayempa.
Snura Mushi.
Snura ameeleza hisia zake hizo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram asubuhi ya leo na kufanya kuwashangaza watu kwa kile alichokiandika, huku wengine wakitaka kupatiwa wao nafasi hiyo ya kumpatia ujauzito.
"Nimetamani mimba ila sijamtamani mwenye kunipa mimba", ameandika Snura.
Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kutoa kauli kama hizo kwani hapo awali alishawahi kusema pia anatamani kumpatia mwanaume atakaye funga naye ndoa watoto wawili ili aweze kukamilisha idadi ya watoto wanne ambao ni ndoto yake aliyekuwa nayo.