Sakata la Lissu: Zitto Kabwe na Saed Kubenea waitwa Kamati ya Maadili ya Bunge

Image result for ZITTO & KUBENEA
New



Spika Ndugai ameagiza Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe na wa Ubungo, Saed Kubenea wafike kwa Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge.

Spika Ndugai ameiagiza Kamati ya Ulinzi kumhoji Saed Kubenea kwa kumtuhumu kulidanganya bunge kuhusu risasi zilizopigwa kwenye gari ya Lissu.

Spika Job Ndugai ameagiza kamati ya Maadili imuhoji Saed Kubenea kuthibitisha uongo wa Spika juu ya tukio la Tundu Lissu

Jumapili kwenye Ibada ya kumuombea Tundu Lissu iliyoendeshwa na Askofu Gwajima, Mbunge Kubenea alidai Tundu Lissu hakupigwa risasi 28-32 kama Spika alivyosema bali alipigwa Risasi 38.
Kubenea: Tundu Lissu amesema anawajua kwa sura waliompiga risasi

UPDATES:

Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amemuagiza kutafutwa kwa namna yoyote Mbunge wa Ubungo(Chadema), Saed Kubenea apelekwe kesho kwenye Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ili ahojiwe kuhusu kauli aliyoitoa ya kumtuhumu Spika kuwa amedanganya idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.

Pia Spika Ndugai ameagiza Kubenea na Mbunge wa Kigoma Mjini(ACT Wazalendo), Zitto Kabwe kupelekwa katika Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka kwa tuhuma mbili tofauti

Zitto anatuhumiwa kutamka kuwa Bunge limewekwa mfukoni na muhimili fulani, wakati Kubenea ni kwa kumtuhumu Spika kusema uongo wa idadi ya risasi alizopigwa Lissu.

Spika Ndugai ametoa maagizo hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumanne.

Chanzo: Mwananchi