Rais Magufuli atoa kamisheni 422

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi Dkt. John Pombe Magufuli, leo amewatunuku kamisheni maafisa wa Jeshi 422 ambao wamehitimu mafunzo mbali mbali kwenye chuo cha Jeshi Monduli mkoani Arusha.
Tukio hilo ambalo limefanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Mjni, limehudhuriwa na viongozi mbali mabali wa kitaifa na mafisa wa Jeshi nchini pamoja na wananchi mbali mbali wa mkoa wa Arusha.
Kabla ya kuwatunuku kamisheni maafisa hao wa jeshi, Rais Magufuli alikagua gwaride maalum, na kutoa zawadi kwa maafisa wa jeshi watano waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo yao.
Tukio hilo la Rais Magufuli kuwapa Kamisheni Maafisa wa Jeshi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni la kwanza kufanyika katika uwanja wa wazi badala ya viwanja vya jeshi wilayani Monduli.