Rais atoa siri kushinda Uchaguzi 2020
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amefunguka na kutoa siri kwa viongozi wa CCM na serikali kuwa wanapaswa kukifanya chama hicho kuzidi kukubalika ili kushinda kwa kiwango cha juu uchaguzi Mkuu ujao 2020
Dk. Shein amesema hayo leo alipokuwa akiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar ambapo amewataka viongozi kutambua umuhimu wao kushuka chini kwa wananchi na kushirikiana nao katika harakati za maendeleo na kubaini changamoto zao ili kuzipatia ufumbuzi na kujenga imani kwa wananchi.
Aidha Dk Sheni alimalizia kwa kusema viongozi wa Chama na Serikali wana wajibu mkubwa wa kutimiza wajibu wao kikamilifu katika kukiwezesha Chama na Serikali kuendelea kukubalika zaidi kwa wananchi na kushinda kwa kiwango cha juu zaidi katika uchaguzi mkuu ujao 2020.
Mbali na hilo kikao hicho kilipokea na kujadili majina ya wagombea 50 waliojitokeza kuomba nafasi za Uenyeviti wa CCM katika Wilaya 12 za Unguja na Pemba na kutoa mapendekezo yake ili kuyapeleka katika vikao husika.
Post a Comment