Mwili wa mtekaji Arusha bado mtihani
Baada ya kuwepo taarifa za familia ya marehemu Samson Peter kugoma kuzika mwili wa kijana huyo ambaye aliwateka na kuwaua watoto wawili, hospitali ya Mt. Meru imesema haijapokea taarifa zozote kuthibitisha hilo na kwamba mwili huo bado wameuhifadhi.
Samson Peter |
Habari zilizopo kutoka kwa msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti Hospitalini hapo, Francis Coster akiongea na kituo kimoja cha TV amesema hakuna ndugu yeyote aliyejitokeza kuja kudai mwili kwaajili ya maziko na wamekuwa wakisikia taarifa za kugomewa mwili huo kutoka kwenye vyombo vya habari.
Aidha amebainisha kuwa taratibu za maziko ya marehemu mbalimbali ambao ndugu zao hawakujitokeza mapema hospitali hufanya taratibu za mazishi baada ya siku 21.
Samsoni alifikwa na mauti kwa kupigwa risasi na Polisi Murieti Jijini Arusha September 6, mwaka huu alipojaribu kutoroka wakati akienda kuwaonyesha askari watu alioshirikiana nao kufanya utekaji na mauaji hayo.
Post a Comment