MAKONDA AWAPA SOMO TRA DAR, AWATAKA WASIKATISHE TAMAA WAFANYABIASHARA.

Baadhi ya wafanyabiashara wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, mhe paul Makonda hayupo  pichani katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo.( picha na Camera ya Mwambawahabari)




Baadhi ya wafanyabiashara wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, mhe paul Makonda hayupo  pichani katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo.( picha na Camera ya Mwambawahabari)

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mhe Paul Makonda ,meitupia lawama Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa kodi Ilala  kwa tabia yao ya kuvizia wafanyabiashara wakati wa ukusanyaji mizigo, na baadhi yao hudai rushwa  ili kuwa kusamehewa faini wanao tozwa na Mamlaka hiyo.


Mhe. Makonda Ameyasema hayo leo katika mkutano wake na Wafanya biashara wa Dar es aliouitisha kuzungumza nao  ili kutatua kero zao.

"Ninaushahidi wa clip hapa m fanya kazi wa TRA akiomba milioni 100 katika duka la mfanyabishara biashara, na ninyi wafanyabiashara Nawaomba  mfunge camera katika maduka yenu ili tuwabaini hao wanao ombarushwa". Amesema Makonda.

Aidha amewaomba wafanyabiashara  kuchangia ujenzi wa shule na Ofisi za walimu  katika mkoa wa Dar es Salaam, na kuwaomba kuunda Kamati  kwaajili ya kujadili maendeleo yao kibiashara na changamoto za kazi yao.

Mkuu wa kodi  mkoa wa kodi Ilala Abdull Mapembe, amesema Kuna baadhi ya wafanyabiashara wa sio waaminifu huzunguka na lisiti moja, pia huandika bei tofauti na thamani hali si ya bidhaa katika lisiti ya kielektroniki.
                                                 
"Ikiwa Mfanyabiashara atabainika kuwepo kulipa kodi au kuandika lisiti kwa kuficha gharama hali si ya mazoez ya bidhaa atachukuliwa hatua za kisheria." Amesema Afisa huyo.

Nao baadhi ya wafanyabiashara biashara waliopata fursa ya kuzungumza katika mkutano huo wamesema Kuna baadhi ya  watumishi wa serikali waache zoom mchezo machafu kwa wafanyabishara na kuwa kati sha tamaa kufanya biashara na wateja kutoka nje ya nchi walio kuwa wa nakuja kununua bidhaa nchini hususani eneo la kariakoo.

Kwaupande wao wafanyabiashara wa vifaa na spea za magari wamemwomba mhe. Makonda kutoa utaratibu kwa Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam  ilikurudisha vifaa vifaa vya magari ambavyo havijachukuliwa na wananchi , nakusema kuwa hii inaonyesha kuwa  havikuwa vya wizi hivyo ni haki kurudishiwa wenyewe.