ma Taarifa iliyotufikia kuhusu Kanisa la Askofu Gwajima

KANISA la Ufufuo na Uzima lililopo Mbezi Inn linalomilikiwa na Askofu Josephat Gwajima limebomolewa. Nyumba hiyo ya ibada ambayo pia ilikuwa ikitumika kama kituo cha maombezi imebomolewa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads).

Imeelezwa kanisa hilo limejengwa ndani ya hifadhi ya Barabara ya Morogoro ya mita 121.5. Kwa mujibu wa waumini wa kanisa hilo, pia limekuwa likitumika  kama kituo cha kufundishia wachungaji limebomolewa jana jioni hali iliyosababisha waumini wa Kanisa hilo kusalia nje. Vitu vikiwa nje na baadhi ya waumini wakiendelea  na maombi nje.