Kubenea aachiwa achague wapi atibiwe

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ambayo leo ilimuhitaji Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea kwa mahojiano imeamua kumuachia Mbunge huyo mpaka pale afya yake itakapoimarika.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao kufanyika  Mwenyekiti Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. George Mkuchika amesema wamejiridhisha kuwa afya ya mbunge huyo haiko sawa, hivyo wameamua kumpa muda wa kupata matibabu, na ataamua mwenyewe wapi atapenda kupatiwa matibabu hayo.
"Kufuatia hali tuliyomuona nayo Mheshimiwa Kubenea na maombi yake ambayo ametaka tumpe muda aendelee na matibabu mpaka pale afya yake itakapoimarika kamati imekubali na imeagiza mara moja mheshimiwa Kubenea apelekwe katika zahanati ya bunge, apatiwe huduma ya kwanza na baadaye yeye mwenyewe ataelekeza au atachagua mahala gani kwenda kupata matibabu”, amesema Mheshimiwa Mkuchika.
Leo asubuhi Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea alifikishwa mjini Dodoma kwenye kamati ya maadili ya Bunge chini ya ulinzi wa polisi