DIWANI WA UKAWA ATUMIA MILIONI 10 KUTATUA CHANGAMOTO SUGU.

Diwani wa Kata ya Tabata kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amelazimika kutumia Milioni 10 kutengeneza Kilima cha Barabata chenye urefu wa mita 30  ambacho kilikuwa kinagharimu maisha ya Wakazi wa tabata.


Kilima hicho kilichopo Mtaa wa tabata mama kiliweza kusababisha vifo vya watu wanne kwa nyakati tofauti baada ya magari kadhaa kushindwa kupanda kilima kutokana na kuwa na miundombinu ambayo sio rafiki.

Akizungumza na wakati wa ufunguzi wa maradi wa ujenzi wa kilima hicho, Diwani wa Kata ya Tabata Patrick John Assenga, amesema kuwa kilima hicho kilikuwa tatizo sugu kwa wakazi wa tabata kwa muda mrefu.

Assenga amesema kuwa licha ya kuleta maafa, wakazi wa tabata walikuwa wanazunguka kutafuta njia rafiki ili waweze kwenda katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Amesema kuwa magari, bajaji pamoja pikipiki (bodaboda) zilikuwa zinashindwa kupanda kilima kutokana na ubovu wa miundombinu, lakini sasa wamefanikiwa kutatua tatizo hilo.

“Kabla sijaingia madarakani uongozi uliokuwepo wakati huo walikuwa wanachangisha fedha kwa wananchi ili kutengeza kilima, lakini 
walishindwa kutokana na kuwepo kwa wajanja” amsema Assenga.

Amesema kuwa walifanikiwa kutumia milioni 16 kwa ajili ya ujenzi huo, lakini walijenga chini ya kiwango na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa tabata.

Amefafanua kuwa baada ya kuingia madarakani kwa kipindi cha muda mfupi ameweza kutatua tatizo hilo ambalo limekuwa likiwasumbua wanachi kwa miaka yote kabla ya uongozi wake.

“Ujenzi wa mradi wa kilima umekamilika ambao ni bora kwa sababu tumetumia vifaa vya kisasa kwa kuweka zege, nondo ili mradi huu hudumu kwa muda mrefu” amesema Assenga.

Hata hivyo ameeleza kuwa ndani ya kata yake kuna mipango mingi ya kimaendele kiwemo kujenga kituo cha afya ambacho kinatarajiwa kuwa msaada katika jimbo la Sengerea kwa kutoa huduma kata 12.

Amesema kuwa mpaka sasa tayari wamepata eneo kwa ajili ya kujenga kituo cha afya na baada ya muda mfupi Manispaa ya Ilala itatenga fedha kwa ajili ya kukamilisha mradi huo.

Assenga amesema ili tuendelee kupiga hataua katika masuala mbalimbali  ni vema Serikali kuludisha kodi ya mabango kwa Halmashauri ya Ilala ambapo awali walikuwa wanakusanya bilioni 15 kwa mwaka na kusaidi kuharakisha maendeleo.

Hata hivyo wananchi wa tabata wameonekana kuwa na furaha kubwa baada ya kuona ujenzi wa kilima cha barabara kukamilika.

Wakizungumza na MWAMBA WA HABARI  wamesema kuwa Diwani wa Kata ya tabata amefanya kazi kubwa kwa muda mfupi kutokana na viongozi waliomtanguliwa wameshindwa kutatua tatizo hilo.

Joyce John Mkazi wa tabata amesema wamama wajawazito, wanafunzi walikuwa wanapata tabu wakati wanapanda mlima huu lakini sasa kila kitu kitakwenda sawa


Diwani wa Kata ya Tabata Patrick John Assenga akikata utepe wakati wa ufunguzi wa kilima hicho kilichopo Mtaa wa tabata mama jijini Dar es Salaam
Diwani wa Kata ya Tabata Patrick John Assenga akizungumza na wakazi wa tabata wakati wa ufunguzi wa mardi wa kilima cha barabra chenye urefu wa mita 30.