CHADEMA wapata pigo Mbeya

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Mbeya kimepata pigo baada ya kumpoteza diwani wa viti Malaam Mhe. Esther Mpwiniza ambaye amefariki jana kwa presha.
Mwenyekiti wa BAVICHA  Wilaya ya Mbarali, Jidawaya Kazamoyo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kuwa Septemba 8, 2017 Esther Mpwiniza alishiriki kutoa tamko la kulaani shambulizi la kinyama na kikatili alilofanyiwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kupigwa risasi na watu wasiojulikana na kusema pia alichangia damu katika ofisi za damu salama Kanda ya Mbeya kuenzi damu aliyomwaga Tundu Lissu.
Aidha Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama 'Jongwe' amesikitishwa na msiba wa diwani huyo na kusema kwake ni pigo kubwa na pigo kwa watu wa Mbeya na wananachama wa CHADEMA kiujumla kutokana uwezo wa diwani huyo na jinsi ambavyo alikuwa akijitoa kwa watu pamoja na kukipigania chama chake.  
"Mh Diwani Esther Mpwiniza kamanda wangu wa nguvu na dada yangu ni msiba mkubwa kwangu, BAWACHA na Jiji la Mbeya" alisema Joseph Mbilinyi.