Apandishwa mahakamani kwa kuolewa

Mkazi mmoja wa Manispaa ya Mtwara Sharifu Issah maarufu kamaZamda Salumu amefikishwa mahakamani kwa kosa la kufanya vitendo vya utovu wa kimaadili kwa kujifanya mwanamke na kumshawishi mwanaume mwenzake kufunga ndoa na kuishi pamoja kama mke na mume.
Akisoma kesi hiyo hakimu mkuu mkazi Richard Kabate amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 157 cha kanuni ya adhabu sura namba 16 ya sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Kabate amedai kuwa mshtakiwa kati ya mwezi Machi mwaka huu na mwezi wa Juni akiwa katika vijiji vya Mkahala na Mpanyani halmashauri ya Nanyambamkoa wa Mtwara kwa makusudi alijifanya mwanamke na kumshawishi Mustapha Saidi Nurdini kwa kumtongoza na kufunga nae ndoa isiyo halali.
Hata hivyo hakimu Kabete amesema kitendo hicho kinatoa tafsiri ya ukiukwaji mkubwa wa maadili kwa watu wa jinsia moja ya kiume kuishi kinyumba.
Mshtakiwa aliposomewa shtaka hilo na wakili wa serikali George Makasi amekana shitaka hilo na upelelezi wa kesi hiyo unaendelea mshtakiwa amerudishwa mahabusu na kesi hiyo itatajwa mahakamani hapo Septemba 28, 2017.