Masauni awataka wananchi kuwafichua wahalifu, aamuru ujenzi wa kituo cha polisi Mbande uanze mara moja

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akizungumza na wananchi wa Mbande, Kata ya Chamazi, Tarafa ya Mbagala,
Wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, wakati alipofanya ziara katika eneo hilo
yenye lengo la kuimarisha ulinzi na usalama katika eneo hilo. Hata hivyo, Masauni
aliamuru ujenzi wa Kituo cha Polisi Mbande ambao utajengwa kwa michango ya
wananchi na Serikali uanze mara moja, na pia aliwataka wananchi kutoa taarifa
kwa kuwafichua askari polisi wanaohisiwa kushirikiana na wahalifu katika eneo
hilo.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia),
akimsikiliza Mkazi wa Mbande, Mbagala, jijini Dar es Salaam, Muhidin Maftaa
alipokua anamuuliza swali kuhusu hali ya ulinzi na usalama katika eneo hilo.
Ambaye alifanya ziara katika eneo hilo yenye lengo la kuimarisha ulinzi na
usalama, aliamuru ujenzi wa Kituo cha Polisi Mbande ambao utajengwa kwa
michango ya wananchi na Serikali uanze mara moja, na pia aliwataka wananchi
kutoa taarifa kwa kuwafichua askari polisi wanaohisiwa kushirikiana na wahalifu
katika eneo hilo.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto),
akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, jijini Dar es Salaam,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Gilles Muroto,alipokuwa anajibu
mswali mbalimbali ya wananchi wa Mtaa wa Magengeni Mbande, Mbagala, jijini
Dar es Salaam. Masauni alifanya ziara katika eneo hilo yenye lengo la kuimarisha
ulinzi na usalama na aliamuru ujenzi wa Kituo cha Polisi Mbande ambao
utajengwa kwa michango ya wananchi na Serikali uanze mara moja, na pia
aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa kuwafichua askari polisi wanaohisiwa
kushirikiana na wahalifu katika eneo hilo.