MANISPAA YA UBUNGO YAZINDUA MAGARI MATANO(5) ( Pick up - HILUX) MAPYA KWA AJILI YA UKUSANYAJI WA MAPATO*


Mkurugenzi wa manispaa ya ubungo akikata utepe ishara ya kufunguliwa kwa magari hayo mapema hivi leo
Hapa wakifurahia kwa pamoja baada ya zoezi la kuzindua kwa magari hayo 
Mkurugenzi wa manispaa ya ubungo akikagua gari kwa ndani tayari kwa kuanza matumizi ya kiutendaji


  Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na Mkurugenzi Ndg. John Lipesi Kayombo imezindua magari matano mapya Aina ya Pick- up Hilux waliyoyanunua kwa fedha za mapato ya ndani ( OWN SOURCE)

Ikiwa ni moja ya mikakati ya awali ya Manispaa hii katika kuboresha mapato ya ndani yatakayoleta maendeleo katika maeneo mbalimbali ya kijamii kama Hospitali, zahanati, shule na Ujenzi wa vituo vya afya magari hayo yote yamepelekwa katika idara ya Fedha na biashara kitengo Cha Mapato.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa magari hayo Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg. John Lipesi Kayombo alisema ununuaji wa magari hayo ni kwa ajili ya kuboresha zaidi ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwa kuzipeleka Gari hizo kwa wakusanyaji wa mapato moja kwa moja ambao wako kwenye kata na mitaa ndani ya Manispaa ya ubungo
"Manispaa ya Ubungo tulikuwa na magari machache sana, ukusanyaji wa mapato ulikuwa ni mzuri lakini tumeona bora tuongeze vitendea kazi ili kufikia lengo letu la kukusanya zaidi shillingi billioni 23 ambayo ndio Bajeti ya 2017/18 ili kutekeleza miradi ya maendeleo kwa asilimia 100 na kuweza kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi" alisema Kayombo. 
Pia Mkurugenzi Kayombo aliwashukuru Madiwani sambamba na watumishi wa Manispaa hiyo kwa ushiriki wao na hatimaye kuweza kuongeza mapato ya Manispaa hiyo.
Akizungumza baada ya uzinduzi na kukabidhiwa magari hayo kwa niaba ya Idara ya fedha mwaka hazina wa Manispaa ya Ubungo Ndg. Jane Machicho alimshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo na menejimenti nzima kwa kutatua changamoto ya usafiri katika ukusanyaji wa mapato kwani itasaidia kuboresha ukusanyaji wa mapato hayo na hatimaye kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato la shilingi billioni 23 kwa mwaka.
Manispaa ya Ubungo tangu kuanzishwa kwake ambapo ni takribani miezi tisa sasa imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuboresha mapato ya manispaa ambapo moja wapo ilikuwa ni kutatua tatizo la usafiri katika ukusanyaji wa mapato katika kata za wilaya ya Ubungo.

Hongera Baraza la Madiwani, Mkurugenzi na menejimenti nzima ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.