MAKONDA : MWANANCHI ALIYEPATA AJALI AKAKATIKA MIGUU AMA MGUU AJE OFISINI KWANGU AJIANDIKISHE TU TAMPATIA MGUU WA BANDIA BURE





Tanzanite blog

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amewataka wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam ambao ni walemavu wa miguu, waliopata miguu wanao hitaji Miguu ya bandia  kwenda kujiandikisha ofisini kwake ili waweze kupatiwa huduma hiyo.

Mhe. Makonda Ameyasema hayo leo ofisini kwake alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuweka wazi kuwa huduma hiyo itatoka bure kwa wananchi wake kwa kuwa huenda Kuna baadhi ya watu wa nahitaji ila waliowaalika uwezo wa kumudu kununua miguu hiyo.

"Nawaomba wananchi wangu mje siku ya juma tatu mjiandikishe na kupima kila mtu mwenye hitaji huo ili tuweze kujua ni kipimo cha mguu wako Kabla  ya kutengenezewa, tutakuwa na miguu aina mbili waliovunjika kuanzia kwenye paja na walio katwa  kuanzia chini zaidi ya hapo " amesema Makonda

Amesema, amepewa kazi ya kuhudumia wananchi makundi yote katika jamii na Mhe. Rais Magufuli anataka kila mwananchi  wa mkoa huo aweze kufaidika na Serikali yake.

"Kuna watu wamekatwa miguu kwa ajali mbalimbali hawana uwezotena wa kufanya shughuli zao lakini tukiwa patia  hii miguu wataweza kurejea katika hali ambayo itawezesha kufanya shughuli zao za kujipatia kipato" amesema Makonda.

Akizungumzia gharama ya miguu hiyo bandia Makonda amesema, kila mguu Utah gharam shilingi million 3 na kwa yote 200 itakuwa ni shilingi milioni 800.