JUMLA YA MANENO YA NAIBU WAZIRI SULEIMAN JAFO ALIYOYASEMA KATIKA ZIARA YAKE KIGAMBONI.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua miradi ya wilaya ya Kigamboni aliyekuwa nyoosha mkono ni Mkurugenzi wa Manispaa spaa ya Kigamboni ndg Stephen Katemba na wa pili kutoka kwa Naibu Waziri ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rachel I Mhando. Mwingine ni Meya wa Kigamboni. 


Serikali imesema itaendelea kusimamia utendaji kazi wa watumishi wa Halmashauri nchini lengo likiwa kuweka usawa wa kuitendaji kuanzia ngazi ya Wilaya mkoa hadi Taifa.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa juma hili na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jafo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika  Wilaya ya Kigamboni iliyokwenda sambamba na mkutano Maalumu na viongozi pamoja na watumishi wa Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine Waziri Jafo amesema utendaji kazi bora utakaofanywa na watumishi wa Kigamboni pamoja na viongozi wao utaufanya Mji huo kuwa wenye maendeleo ukilinganisha na maeneo mengine.

Miongoni mwa miradi ya Maendeleo ambayo Naibu Waziri Jafo ameyatembelea ni Pamoja ujenzi wa mabweni kwaajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita wa Shule ya Sekondari Nguva. 
Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni iliyopo vijibweni ambapo akiwa shule ya Sekondari nguvu Naibu Waziri Jafo amewataka wanafunzi kuongeza bidii kwenye masomo ili wapate matokeo mazuri kwenye mitihani ya Taifa.

Aidha amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Stephen Katemba  kukaana menejimenti yake kuona namna ya kujenga duka kubwa la dawa litakalo  hudumia  wanachama wa bima ya Afya ambao kwa sasa wanapata shida kutokana  na kila mara kuandika kujua dawa nje ya hospitali.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Manispaa hiyo Bakari Mbwana Amemwambia Waziri Jafo kuwa upungufu wa Dawa unasababishwa na idadi kubwa ya wanachi  ukilinganisha na bajeti wanayo pewa  ambapo kwa mujibu wa bajeti hiyo ni wa tu Laki mbili tu ndo walitoa kuwa kuhudumia huku kukutwa na wananchi Zaidi ya Laki tano wanaotegemea kupatiwa huduma katika Hospital hiyo. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni ndg Stephen Katemba  alimhikikishia Waziri Jafo kuwa maagizo yote aliyoyatoa atayafanyiakazi.