HAYA HAPA WALIYOYASEMA WANANCHI KUHUSU MANISPAA YA UBUNGO KUN'GARA KATIKA MAONESHO YA 8 8/2017.



Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo yadaiwa kun'gara katika maonesho ya nanenane na kufanya vizuri ukizingatia ni ushiriki wake wa kwanza katika maonesho haya.

Wananchi waliohojiwa na Afisa habari wetu kutoa maoni yao juu ya sherehe za nanenane wameiongelea Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kama halmashauri iliyon'gara kwa maandalizi mazuri na ya kuvutia ambapo wamenufaika nayo.

"Kwa kweli kwanza sikutegemea kuona hali ninayoiona katika banda hili la Ubungo ,Ubungo mmejipanga ,tumeelimika vya kutosha na tumeshuhudia teknolojia za ajabu hasa hii ya usafishaji wa maji imenivutia zaidi,hongereni sana"alisema Ramadhani Mweisige mkazi wa temboni alietembelea mabanda ya Ubungo.

Si yeye tu maoni mengi yametolewa na wananchi mbalimbali wakishukuru kwa elimu ya kilimo cha mbogamboga,ufugaji,elimu ya usindikaji wa vyakula nk.

Si hayo tu teknolojia ya mitambo ya kuzalisha umeme ni moja ya kivutio kilichowavutia watu katika banda la Ubungo na utengenezaji wa magogo ya kupikia kwa kutumia taka.

Tunashukuru wananchi wetu mliotuma pongezi na maoni mbalimbali kupitia mitandao yetu ya Facebook,Instagram twitter na wale waliosubscribe na kulike Ubungo municipal online TV .Aidha wote waliotembelea banda letu viongozi mbalimbali wananchi,makundi mbalimbali ya kijamii asanteni na karibuni sana.

Sherehe za nanenane kwa kanda ya Mashariki ambapo na Ubungo ipoj ndani ziliambatana na burudani mbalimbali na mgeni rasmi katika kilele alikuwa Waziri wa afya,Maendeleoya jamii,ustawi wa jamii,jinsia,wazee na watoto Dkt.Khamis Kigwangala.Mikoa iliyojumuisha Kanda hii ni Tanga,Pwani,Dar es salaam,Morogoro.

Sherehe hizi hufanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kitaifa zimefanyika mkoani Lindi na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiwa mgeni rasmi,ambapo kwa mwaka huu ujumbe ulikuwa "Zalisha kwa tija mazao  na bidhaa za kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi wa kati.

Hongereni Manispaa ya Ubungo chini ya uongozi wake Mkurugenzi makini  Ndg.John L.Kayombo  na kila la kheri kwa maandalizi yajayo.

#UBUNGO YATOFAUTI

IMETOLEWA NA KITENGO CHA UHUSIANO -UMC