Cuf Yatoa Ufafanuzi Uamuzi Wa Mahakama Kuu Juu Ya Kesi Ya Wabunge Nane Na Madiwani Wawili.
Chama
cha Wananchi (CUF) kimeshangazwa na hatua ya Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini kuendelea kumtambua Mwenyekiti wa Chama hicho, Prof. Ibrahim
Lipumba kwakuwa alijiuzuru kwa hiari yake na kutimkia nje ya nchi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na Naibu Mkurugenzi wa
Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Bw. Mbarala Maharagande, alisema
kitendo hicho kinavunja na kukiuka Katiba ya chama hicho.
Alisema
chama tayali kimefungua kesi kwaajili ya kutaka kujua ametumia vifungu
gani kuendelea kumtambua Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim
Lipumba aliyekuwa amejiuzuru kwa hiyali yake mwenyewe Sambamba
wamefungua kesi nyingine dhidi ya Mwenyekiti huyo ya kuhoji uhalali wa
kuwafukuza uanachama wabunge wanane na madiwani wawili wa chama hicho,
kitu ambacho kimesababisha taharuki ndani ya chama.
Alisema kufatia kuvuliwa uanachama wabunge na madiwani na
Lipumba walifungua shauri la msingi mahakama kuu (CIVIL CASE
NO.143/2017) lakini pia kuna maombi madogo (Miscelleneous Civil
Application No. 447/2017) ambayo inahusiana na kuomba Zuio la muda
(Temporary Injuction Order and To maintain Status Quo)ambalo
limeripotiwa ndivyo sivyo na kuleta sintofahamu kubwa kwa jamii pamoja
na wanachama wa chama hicho.
Akitolea ufafanuzi shauri hilo Bw. Maharagande alisemaShauri
la msingi (CIVIL CASE NO. 143/2017) Limepangwa kusikilizwa/kutajwa
Tarehe 31/8/2017, ambapo kimsingi Wabunge na Madiwani wanadai haki ya
uanachama wao kwa kuhoji mchakato uliotumika kufikia maamuzi hayo ambao
haukufuata katiba ya CUF na huku kukiwa na mashauri ya msingi
yanayoendelea mahakamani.
Alisema
wabunge hao Wanahoji juu ya uhalali wa vyombo vilivyochukua hatua hizo
za nidhamu dhidi yao kama zimefuata taratibu ikiwa ni pamoja na
kuwapatia taarifa za tuhuma zao kwa maandishi ili waweze kujiandaa kwa
utetezi, siku na tarehe ya kikao hicho ukizingatia kuwa si wote
wanaoishi hapa Dar es Salaam.
Bw.
Maharagande Aliongeza kuwa wameshtushwa na uharaka wa Bunge na Tume ya
Taifa ya Uchaguzi kuchukua hatua bila kujiridhisha na wala kuwauliza na
kujua kutoka kwao kilichojitokeza, kwa ujumla hawakupewa nafasi ya
kusikilizwa na kujitetea.
Alisema
kwa maamuzi huo tayali umekiuka katiba ya chama hicho kwa kushindwa
kuzingatia haki za kikatiba ikiwemo kukata Rufaa ndani ya siku 14 Ibara
ya 108(5) ya katiba ya CUF, ambapo Wabunge hao tayali wamekatia Rufaa
maamuzi huo na kuandikia barua na kukiomba Chama kupitia Katibu Mkuu
kiweze kuitisha Mkutano Mkuu wa Taifa ili kufikisha rufaa yao.
“Mkutano
Mkuu ndio wenye mamlaka na maamuzi ya mwisho juu ya masuala yote ndani
ya Chama utolewa uhamuzi kama Lipumba na wenzake pale Baraza Kuu la
uongozi taifa lilipowachukulia hatua za kinidhamu kwa kuwasimamisha
uanachama Tarehe 28 Agosti, 2017” alisema Maharagande.
Kuhusu
hatma ya shauri dogo ambalo limefunguliwa na wabunge nane na madiwani
wawili ambalo lilitajwa tarehe 2 mwezi huu Bw. Maharagande alisema
waliomba Mahakama Kuu itoe zuio la muda (Temporary Injuction Order and
to maintain Status Quo) kusimamisha maamuzi ya bunge na tume na
kuwarejesha wabunge waliovuliwa uanachama waendelee na shughuli za bunge
na kuwawakilishi halali mpaka hapo shauri la msingi
litakapoamuriwa.
litakapoamuriwa.
Alisema
Kabla maombi hayo hayajasikilizwa Walalamikiwa (Respondent's
No.1,2,3,4,5,8-15)waliweka Pingamizi la Awali (Preliminary Objections)
juu ya shauri hilo kwa madai ya kukosa sifa za kisheria (incompetence
enacted provisions of law) na hoja hizo 4 za pingamizi zilizosikilizwa
takribani kwa masaa 4 Tarehe hiyo 2/8/2017 pale shauri hilo lilipoitwa
kwa kusikilizwa na baadae kupangwa kutolewa maamuzi ya Pingamizi hilo
jana Tarehe 4/8/2017.
“Pingamizi
juu ya maombi ya Shauri namba 447/2017 yameondolewa mbele ya Mahakama
na wala hakuna hiko kitu kinachoitwa ‘kesi imefutwa, au kutupiliwa mbali
au mahakama imeruhusu Wabunge wapya kuapishwa, KWA HAKIKA HAKUNA
USHINDI WA MAAMUZI YALIYOTOLEWA’ kama inavyoripotiwa” Aliongeza Bw.
Maharagande.
Alisema Maamuzi hayo ya mahakama kuu yamewapa fursa ya kuandaa vizuri zaidi nyaraka hizo na tayari tumepata faida ya kujua hoja wanazosimamia walalamikiwa (Respondents) Wabunge tayari wameshaandaa nyaraka zilitayarishwa na kusainiwa zikiwa na marekebisho yote ya msingi na ya lazima yaliyopaswa kuingizwa ikiwemo kuwajumuisha katika shauri hilo Wakurugenzi wa Manispaa za Ubungo na Temeke ambao wanahusika kutokana na Madiwani waliopo katika halmashauri zao.
Alisema Maamuzi hayo ya mahakama kuu yamewapa fursa ya kuandaa vizuri zaidi nyaraka hizo na tayari tumepata faida ya kujua hoja wanazosimamia walalamikiwa (Respondents) Wabunge tayari wameshaandaa nyaraka zilitayarishwa na kusainiwa zikiwa na marekebisho yote ya msingi na ya lazima yaliyopaswa kuingizwa ikiwemo kuwajumuisha katika shauri hilo Wakurugenzi wa Manispaa za Ubungo na Temeke ambao wanahusika kutokana na Madiwani waliopo katika halmashauri zao.
Aidha Bw, maharagande ametoa wito waandishi wa habari kuripoti habari za kimahakama kwa uashihi na kutumia weledi ili kuepusha taharuki na kuwachanganya wananchi na wadau na kuacha kuripoti taarifa kwa kutumia ‘ushabiki’ kwani mkanganyiko kwa kufanya hivyo haukujengi weledi na afya njema kwa kuwahabarisha wananchi ndivyo sivyo.
Pia amewataka wanachama wa CUF, Wapenzi na Watanzania kwa ujumla kupuuza habari za upotoshaji na propaganda kwani si shauri la msingi wala maombi ya zuio lililosikilizwa na Mahakama Kuu na kuyatolea maamuzi bali Kilichotolewa maamuzi ni Pingamizi juu ya hoja za kisheria pekee ambazo zimesharekebishwa na kurejesha upya shauri hilo mahakamani.
Post a Comment