ZIFF Kuwashindanisha Darasa, Rayvanny, Jux na wengine kutoka Kenya na Uganda
Kampuni ya Wanene Entertainment kwa kushirikiana na Tamasha la nchi za
Jahazi (ZIFF) wamesaini makubaliano ya kudhamini kipengele cha video
bora ya Afrika Mashariki, ambapo mshindi wa kipengele hicho atapata
fursa ya kurekodiwa na kutengenezewa video bure na kampuni ya Wanene
Entertainment.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa
Masoko kutoka ZIFF Isihaka Mlawa amesema ZIFF wanayofuraha kubwa kwa
kampuni ya Wanene Entertainment kudhamini kipengele cha video bora ya
Afrika Mashariki, itakayo zishirikisha nchi tatu za Tanzania, Uganda na
Kenya.
Mlawa ameeleza kuwa kwa miaka mingi ZIFF ilikuwa imejikita upande mmoja
wa filamu, ndiyo maana wakaamua kuanzisha kipengele hicho ambapo kwa
mwaka jana alishinda Fid Q na video yake ya Walk it Off ambayo
ilirekodiwa nje ya Tanzania, ila kwa mwaka huu video zote zilizo
chaguliwa zimerekodiwa na kufanyiwa video na waandaaji na waongozi
kutoka kwenye nchi zao.
Mlawa amewataja wasanii wanao shindanishwa katika kipengele hicho cha
Video Bora ya Afrika Mashariki kuwa ni Rayvanny kutoka Tanzania na wimbo
wake ya Natafuta Kiki, Darasa na wimbo wake ya Muziki na Jux na wimbo
wake ya Umenikamata, kutoka Uganda ni Eddy Kenzo na wimbo wake ya
Jubilation, Sheebah Karungi na wimbo wake wa Nkwatako pamoja na A Pass
na wimbo wake wa Gamululu, huku kutoka Kenya msanii Everlast na wimbo
wake Gudigudi, Aviril na wimbo wake wa Uko, Nai Boi na wimbo wake wa
Problem huku Nyashinski akishindanishwa kwa wimbo wake wa Now You
Know.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wanene Entertainment Darsh Pandit
ameeleza kuwa wameamua kudhamini kipengele hicho ili kuyatangaza maeneo
ya Tanzania na Afrika kwa ujumla kwani video itafanyika hapa nchini,
pia itakuwa ni sababu ya wasanii kutoka nje kuja kufanya kazi kwenye
mazingira ya Tanzania.
Pandit ameongeza kuwa wamejipanga kufanya video nzuri kwa mshindi
atakayeshinda tuzo hiyo kwani wanavifaa vya kisasa kwa ajili ya kazi
hiyo.
Wanene Entertainment wanajihusisha na masuala mbalimbali ya uzalishaji
wa video na audio, matangazo na kusimamia wasanii ambapo msanii Chin
Bees ni moja ya wasanii ambao wamefanya kazi na kampuni hiyo na video
yake ya Pepeta.
Post a Comment