WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA NA KUPONGEZA KIWANDA CHA NEMERA NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZAO

 
Kisigino habari
    Waziri mkuu Kassim Majaliwa leo ametembelea viwanda viwili vilivyo chini ya kampuni ya Nemela Group of industries Inayomiliki viwanda vya NEMERA na NIDA jijini dar es salam,Ambapo ameridhishwa na uwekezwaji uliofanywa na Uongoji wa kampuni hiyo.

    zizungumza jijini dar es salam Waziri mkuu kassim majaliwa amesema juhudi za Tanzania ya viwanda imefanikiwa kwa asilimia kubwa kwani wawekezaji wengi pamoja na watanzania wanajitahidi kuanzisha viwanda hapa nchini huku akieleza kuwa mkoa wa dar es salam kuna viwanda takribani 1845 ambavyo vimeajri watanzania wengi.
 WAFANYAKAZI WALIOAJRIWA NA KAMPUNI YA NEMERA PAMOJA  NA NIDA PICHA ILIYO JUU


 .   Waziri mkuu Kassim Majaliwa amevipongeza viwanda vya NEMERA na NIDA kwa kutoa ujuzi kwa wafanyakazi ambao waliingia kwenye ajira bila kuwa na ufahamu wa mambo mbali mbali ikiwemo kuzitumia mashine za kufumia mikeka na kushona nguo.


Waziri mkuu Kassim Majaliwa amechukua fursa ya kuzungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha 
nida nilichopo Tabata jijini dar es salam,Ambapo ametumia nafasi hiyo kuwasihi wafanya kazi hao kutumia fursa vizuri ya kufanya kazi katika kiwanda hicho cha NIDA kwa uadilifu na uaminifu ili wawe mabalozi wema na Tanzania ipate sifa ya kuwa na wafanyakazi waadilifu jambo ambalo linavutia wawekezaji wengine.

       Kwa upande wa wawakilishi wa wafanyakazi hao Ahmed Kiumbe alimuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kushughulikia suala la nyongeza ya mshahara kima cha chini 150,000 ili waweze kumudu gharama za maisha kwani kiwango wanacholipwa na kampuni hiyo kwasasa hakitoshi kiwango cha 800,00 mpaka 100,000 jambo linalopelekea wao kuishi maisha magumu.



 "Mwaka jana alikuja Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde na alituhaidi kulishughulikia suala la nyiongeza ya mshahara alipotembelea kiwanda hiki lakini mpaka sasa tunaona kimya na kiwango ni kilekile" Alisema Kiumbe muwakilishi wa wafanyakazi NIDA. 

        Akijibu suala hilo Waziri Mkuu Majaliwa ameeleza kuwa atamuagiza Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde ili siku ya Jumatatu aje kuzungumza na wafanyakazi hao na kuangalia namna gani wanaweza kulitatua suala hilo lenye maslahi ya wafanyakazi.

  
Pia amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Muhammad Hamza kushughulikia changamoto hiyo na kuendelea na upanuzi wa kiwanda hicho kwa faidia yao na watanzania kwa ujumla.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (Kulia) akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Namara Group of Industries Muhammad Hamza.
    Ziara hiyo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mbando, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, Naibu Mstahiki Meya Wilaya ya Ilala Omary Kumbilamoto na viongozi mbalimbali.


       Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mstahiki Meya Wilaya ya Ilala Omary Kumbilamoto leo katika ziara yake jijini Dar es Salaam,


 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (Kulia) na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Edward Mpogolo katika ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo alipotembelea kiwanda cha Namera Group of Industries.