Waziri Mahiga atoa majibu kuhusu Tanzania kuinWAZIRI MAHINGA ATOA MAJIBU KUHUSU TANZANIA KUINGILIA UCHAGUZI WA KENYA,AMEWATAJA HAWA KUWA CHANZO


Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam Waziri Mahiga amekanusha tuhuma hizo kwa Tanzania na kueleza kuwa Tanzania haijawahi kuingilia masuala ya kisiasa hususani ya uchaguzi na haitothubutu kufanya hivyo.
Waziri Mahiga amefafanua kuwa taarifa hizi zinazushwa na wabunge wa upinzani wa Kenya na viongozi wa upinzani wa nchini Tanzania, ambapo amesisitiza kuwa serikali itachukua hatua kwa wale wote wanasambaza taarifa hizo zisizo kuwa na dhamira njema ya urafiki katika ya Tanzania na nchi ya jirani ya Kenya.

Zkiwa zimebaki wiki mbili kufanyika kwa uchaguzi wa nchini Kenya Waziri Mahiga amewatakia kila la heri wakenya katika uchaguzi wao.