MKUTANO WA KIMATAIFA WA SHUKRANI KUFANYIKA KESHO UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM
Muhubiri
wa Kimataifa Dk.Nicku Kyungu akihubiri katika kongamano la siku mbili
la viongozi wa dini lilifanyika Kanisa la Naoith Pentekoste Church
Makuburi jijini Dar es Salaam leo kwa Askofu Dk. David Mwasota.
Kongamano hilo linakwenda sanjari na mkutano wa kitaifa wa shukrani wa
kuliombea taifa na Rais Dk.John Magufuli utakaofanyika kesho Uwanja wa
Uhuru.
Mtumishi wa Mungu Askofu Mwaka kutoka nchini Zambia akihubiri katika kongamano hilo.
Askofu Timoth Joseph kutoka nchini Nigeria akihubiri na kufundisha neno la mungu katika kongamano hilo.
Maaskofu na watumishi wa mungu wakiwa meza kuu wakati wa kongamano hilo.
Maombi yakifanyika.
Mchungaji Dk. William Kopwe wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania , kutoka Dodoma akiwa katika kongamano hilo na mkewe.
Viongozi wa dini maaskofu na wachungaji wakiwa kwenye kongamano hilo.
Maombi yakiendelea.
Kongamano likiendelea.
Taswira ya kongamano hilo.
Mwonekano katika kongamano.
Watumishi wa mungu wakiwa katika maombi.
Utulivu katika kongamano hilo.
Na Dotto Mwaibale
KESHO
Jumamosi maaskofu mbalimbali, viongozi wa serikali na taasisi na
viongozi wa dini na wananchi watakutana Uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya maombi ya kitaifa ya shukrani ya kuiombea nchi na
Rais Dk.John Magufuli.
Maombi
hayo ya kihistoria yameandaliwa na viongozi wa dini kutoka madhehebu
mbalimbali ya Huduma Tanzania na Taasisi ya I Go Africa For Jesus.
Katika maombi hayo yatakayofanyika kesho watumishi wa mungu kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwepo maaskofu watahudhuria.
Lengo
kubwa la maombi hayo ni kuiombea nchi amani na kumuunga mkono rais
Dk.Magufuli ambaye amekuwa akiomba watanzania wamuombee mara kwa mara.
Kabla
ya maombi hayo kwa jana na leo lilifanyika kongamano la viongozi wa dini
ambapo watumishi wa mungu mbalimbali waliweza kufundisha mambo ya
kiroho na somo la uaminifu na utunzaji wa fedha.
Muhubiri
wa kimataifa ‘Mama Afrika’ Dk.Nicku Kyungu ameomba wananchi, viongozi
wa dini kufika kuhudhuria maombi hayo bila kujali dini ya mtu kwani ni
ya muhimu kwa nchi.
Alisema
maombi hayo yanatoa fursa kwa kila mwananchi ya kuliombea taifa na kuwa
yataanza saa tatu asubuhi hadi mchana ambapo kwaya mbalimbali zitakuwa
zikitoa burudani ya nyimbo za kumtukuza mungu.
Post a Comment