JAMII YA WATU AMBAO VIDOLE VYA WAFIWA HUKATWA
Utamaduni wa watu duniani unatofautiana, moja ya story ambazo sikuwahi kufahamu ni juu ya huu utamaduni wa jamii ya watu wa Dani iliyoko Magharibi mwa Papua, New Guinea.
Ambapo utamaduni wao unahusisha inapotoke msiba wa ndugu yoyote basi ndugu wa marehemu wanaomboleza kwa kujikata vidole.
Hii imeshtua wengi walioisikia, kwa wale waliobahatika kuitembelea basi
ni mashuhuda kwamba watu wengi wa kutoka jamii hiyo wamekatwa vidole na
ndugu yoyote wa marehemu anakatwa vidole, umri sio kitu kinachoangaliwa
sana hivyo hata watoto pia wanaguswa na hii moja kwa moja.
Hapa vidole vinakatwa kwa shoka, vipande vilivyokatwa vinachomwa moto
halafu majivu yanahifadhiwa au kuzikwa pamoja na mwili wa marehemu.
Utaratibu
huo huwa unakuwa na ibada ya utangulizi ili kufukuza mapepo ya marehemu
halafu linafuatia zoezi la kukata vidole, kwa utamaduni huo maumivu ya
mwili huonyesha huzuni ya kufiwa pamoja na kuonyesha upendo kwa
marehemu.
Jitihada zimeanza kufanywa ili kuzuia utamaduni huo ambao madhara yake yameanza kuonekana kwa sasa
Post a Comment