APRM yazinduliwa leo hii.

Makamu wa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Saima Suluhu Hassan amezindua ripoti ya APRM (aAfrica Peer Reviw Mechanism) iliyo kuwa na lengo la kujitathmini maeneo yenye matatizo ili kuona jinsi gani wanayapatia ufumbuzi.



Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.

Ripoti hiyo hasa ilhusu tathmini ya utawala bora inayofanywa na wataalamu wa ndani ya nchi na ule unaofanywa na wataalam wa nje ya nchi ambapo  mchakato huo pia ulihusu utafiti wa mkataba unaolenga kupata takwimu na maelezo mengine juu ya hali halisi ya utawala bora.
Mchakato huu pia ulihusisha wananchi katika kutoa maoni yao kwa kutumia hojaji ya kaya na hojaji ya wataalamu.




Akizungumza mapema leo hii Makamu wa Raisi wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amesema mambo ambayo wamebaini katika ripoti hiyo na maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ni masuala ya rushwa ambalo tayari limepewa kipaumbele kwa kiasi kikubwa,uadilifu,na uboreshwaji wa elimu.

Aidha amesema kuzindua kwa ripoti hii kunamaanisha kuanza kwa mpango mkakati wa kufanyiwa kazi dosari zote ambazo wamezigundua katika tathmini hiyo, kwa maslahi ya taifa.